KAMA UNASUMBULIWA NA MAUMIVU YA KICHWA SOMA HAPA
Maumivu ya kichwa ni hali inayosumbua watu wengi kwa sasa, hii ni kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ambayo yanakuja na dalili za kichwa kuuma, uchovu wa kila siku, hewa nzito ya carbon dioxide na kelele nyingi za viwandani na magari.
Baadhi ya magonjwa na tabia zinayosababisha kichwa kuuma ni kama zifuatazo.
1. Utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe.
2. Magonjwa ya macho mfano refractive errors
3. Magonjwa ya ubongo mfano i.e meningitis
4. Uvimbe ndani ya ubongo i.e brain tumour
5. Magonjwa ya mifupa ya usoni i.e sinusitis
6. Cervical degenerative osteoporosis i.e magonjwa ya mifupa ya uti wa mgongo
7. Magonjwa ya moyo i.e presha ya damu
8. Mgandamizo wa mawazo.
Matibabu ya kiasili
Kutibu chanzo yaani ugonjwa uliosababisha kichwa kuuma ndio njia bora ya kutibu maumivu ya kichwa.
Kama chanzo cha maumivu ya kichwa hayafahamiki njia zifuatazo zinaweza kutibu dalili na kupunguza maumivu hayo.
Kukandwa na kutomaswa na maji ya moto nyuma ya shingo.{ hot compresses and massages.}Kula chakula kisicho na nyama na chenye chumvi kidogo sana.{ vegetarian diet}Weka kitambaa cha maji ya uvuguvugu kwenye paji la uso kuongeza mzunguko wa damu.Tembea sehemu yenye uwazi mkubwa na hewa ya kutosha.Fanya mazoezi ya kuogelea.Ungea na daktari au mwanasaikolojia ambaye anaweza kuatambua ugonjwa wa akili ambao unasababisha maumivu hayo.Pata mda mrefu wa kupumzika na kupata usingizi wa kutosha.
Matibabu ya dawa za kisasa.
Unaweza kutumia dawa ya maumivu kama diclofenac, paracetamol, ibuprofen na kadhalika pale maumivu yanapokua makali sana.bonyeza haya maneno ya kijani kusoma zaidi.
Maoni
Chapisha Maoni