Ugonjwa Wa Kukojoa Damu (Haematuria)
HAEMATURIA ni ugonjwa wa kukojoa damu ambapo kwenye mkojo kunakuwepo chembechembe za damu nyekundu (Red blood cells).
Kukojoa damu ni dalili ya kuonyesha kuwa mtu anayekojoa ana magonjwa katika mfumo wa mkojo kama vile magonjwa ya kichocho au magonjwa mengine yanayoshambulia kibofu cha mkojo au kwenye figo.
SABABU
Magonjwa yanayoshambulia mfumo wa mkojo kama vile UTI, magonjwa ya zinaa hasa kwa wanawake, vijidudu kama staphylococcus saprophyticus, mawe kwenye figo (kidney stone) kuvimba kwa tezi zinazozalisha manii kwa wanaume ambao umri umeenda yaani wazee.
Sababu nyingine ni kama kupata ajali na kuumia sehemu za mfumo wa mkojo (trauma), kupata magonjwa kama kansa ya kibofu cha mkojo, hii hutokea mara nyingi hasa vijijini ambapo watu wanacheza au kuogelea kwenye madimbwi ya maji yasiyotembea.
Sababu zingine ni mtu kuugua magonjwa ya sickle cell anemia na magonjwa mengine ya figo kama vile nephotic syndrome na mengine mengi ambayo yanajulikana kwa kitaalamu na siyo rahisi kuyafafanua kwa Kiswahili.
AINA YA UGONJWA WA KUKOJOA DAMU
Kuna aina mbili za damu kutoka kwenye mkojo, moja ni ile ambayo damu huchuruzika na kuonekana vizuri kwenye mkojo. Hii hujulikana kama macroscopic haematuria au gross haematuria ambayo hutokea kwa wagonjwa wa kichocho au waliopata ajali.
Nyingine ni ile inayoonekana kwa mbali na mara nyingine huonekana wakati mgonjwa anapopimwa mkojo, aina hii hujulikana kama microscopic haematuria.
JINSI YA KUGUNDUA TATIZO (diagnosis)
Mara nyingi tatizo la kukojoa damu hugundulika baada ya mgonjwa kwenda hospitalini na kuonana na daktari na akachukua maelezo yake vizuri na kuagiza mgonjwa akapime mkojo.
Kipimo cha Ultrasound pia husaidia kujua tatizo linalosababisha mgonjwa akojoe damu.
Mashine ya X- ray husaidia kugundua kama mgonjwa ana mawe kwenye figo. Kipimo kingine cha kisasa ni CT scan hiki kina uhakika ila ni ghali sana na hupatikana kwenye hospitali kubwa.
TIBA
Tiba ya uhakika ni kujua sababu inayosababisha mgonjwa akojoe damu kama ni kichocho basi mgonjwa atapewa dawa ya kichocho na kama ni UTI mgonjwa atapewa dawa husika na kama ni magonjwa ya zinaa nayo yatatibiwa. Magonjwa mengine ni kama yale ya figo basi nayo yakigundulika yatatibiwa.
USHAURI
Watoto wasichezee maji yaliyosimama hasa kwenye mabwawa vijijini na mijini, wakigundulika kuwa walicheza basi haraka wapelekwe hospitali kupimwa.
I have understand lakini Mimi nikikojoa mwisho ndoo damu inaroka kwa mbali
JibuFutaMm nimeipata hili matatizo leo nida ya saa tisa alfajiri nimejisikia kukojoa ila mkono unatoka kidogo na unatoka mwanao mtamu ilaunaishia na maumivu na najisikia kwenda kukojoa mara kwa mara na kujua damu
JibuFuta