Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2017

KAMA UNASUMBULIWA NA MAUMIVU YA KICHWA SOMA HAPA

Picha
Maumivu ya kichwa ni hali inayosumbua watu wengi kwa sasa, hii ni kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ambayo yanakuja na dalili za kichwa kuuma, uchovu wa kila siku, hewa nzito ya carbon dioxide na kelele nyingi za viwandani na magari.  Baadhi ya magonjwa na tabia zinayosababisha kichwa kuuma ni kama zifuatazo.   1. Utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe.   2. Magonjwa ya macho mfano  refractive errors   3. Magonjwa ya ubongo mfano i.e meningitis   4. Uvimbe ndani ya ubongo i.e brain tumour   5. Magonjwa ya mifupa ya usoni i.e sinusitis   6. Cervical degenerative osteoporosis i.e magonjwa ya mifupa ya uti wa mgongo   7. Magonjwa ya moyo i.e presha ya damu   8. Mgandamizo wa mawazo.  Matibabu ya kiasili   Kutibu chanzo yaani ugonjwa uliosababisha kichwa kuuma ndio njia bora ya kutibu maumivu ya kichwa.  Kama chanzo cha maumivu ya kichwa hayafahamiki njia zifuatazo zina...

MAUMIVU YA TUMBO

Picha
Maumivu ya tumbo ni dalili inayosumbua watu wengi kwa wakati na umri tofauti. Karibu kila mtu katika maisha yake atapata namna fulani ya maumivu ya tumbo. Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha maumivu ya tumbo na mara nyingi huwa sio za kutisha, hutubiwa na kupona. Mara chache husababishwa na hali ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yako. Maumivu yanaweza kuwa katika sehemu maalum ya tumbo au tumbo zima.  Maumivu Ya Tumbo   Ni vizuri ukijua aina ya maumivu ya tumbo unayopata pamoja na dalili zinazoambatana nayo. Hii itasaidia kujua sababu ya maumivu na katika matibabu. Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa maumivu ya kuchoma, kuungua, kukandamiza, kukata au. Yanaweza kuwa yanakuja na kuacha baada ya muda fulani. Pia yanaweza kuambata na dalili nyingine kama kutapika, kuharisha, kukosa choo, kupata choo chenye damu, tumbo kuvimba na homa.  Sababu za Maumivu ya Tumbo   Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumiv...

BIZARI: KIUNGO CHA MBOGA CHENYE FAIDA NYINGI

Picha
Inawezekana katika maisha yako hujawahi kula mboga iliyowekwa kiungo kinachoitwa bizari, kama umewahi, inawezekana pia hujawahi kujua faida zake mwilini.  Bizari (Turmeric) ni kiungo cha mboga jamii ya mimea unaochimbwa kama mizizi, mfano wa tangawizi, lakini tangawizi yenyewe ina rangi ya njano na hujulikana pia kama ‘manjano’ kutokana na rangi yake.  Kiungo hiki kinatumiwa sana katika Bara la Asia na hasa India na China. Kutokana na umuhimu wake kiafya, vyakula vingi hupikwa kwa kuchanganya na kiungo hiki ambacho sasa kimeenea dunia nzima, ikiwemo Tanzania.  FAIDA ZA BIZARI KIAFYA   Bizari hutumika na watu wengi kama kiungo cha mboga cha kuongeza ladha katika mchuzi na pengine kuweka rangi, lakini kuna faida nyingi unazozipata unapotumia kiungo hiki kila mara katika mapishi yako.  Inaelezwa kuwa bizari ina virutubisho vyenye uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili, mara 8 zaidi ya Vitamin C na Vitamin E, ina uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu (cholesterol) ...

Dalili za Ugonjwa wa zinaa - kisonono

Picha
Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao.  Ugonjwa wa kisonono kwa mara nyingi huwapata vijana na watu wazima. Waathirika wengi wa ugonjwa huu wa kisonono huambatana na magonjwa mengine ya zinaa, kwasababu kunabaadhi ya magonjwa mengine ya zinaa hujificha bila kuonyesha dalili, hivyo kukuta ukiugulia ndani kwa ndani.  Ugonjwa wa kisonono, unazuilika na kutibika pia, unaposikia dalili zozote za magonjwa ya zinaa, unashauriwa kumchukua mwenzi wakona kuwahi hospitali  kuchukua vipimo kwaajili ya matibabu.  DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO.   Mara nyingi ugonjwa wa kisosnono huwa hauonyeshi dalili yoyote mwanzoni. Lakini ukionyesha dalili basi kwa mwanaume utasikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuambatana na usaha kutoka uumeni, kwa mwanamke pia ...

Vyakula Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume

Picha
Mbegu za Flax (Flax seeds):     Wanaume wanapaswa kufahamu aina ya vyakula ambavyo si rafiki kwao katika kuongeza kiwango cha homoni ya kiume iitwayo testosterone inayochochea sifa ya mwanaume yaani kuwa na nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula visivyofaa kuliwa na mwanaume aliyetaka kuwa na nguvu za kiume ni vile vyenye asili ya homoni ya kike iitwayo estrogen. Hivyo sio kila vyakula vinafaa kwa mwanaume eti ilimradi tu vyakula hivyo vinasaidia kujenga mwili au kujaza tumbo wakati mtu akiwa na njaa.  Vyakula visivyofaa kabisa kuliwa na mwanaume kutokana na vyakula hivyo kupunguza homoni ya testosterone ni hivi vifuatavyo:  vyakula vinavyotengenezwa kutokana na unga wa mbegu za flax vimekuwa vikisifiwa kwa kuwa Omega-3 fats ambayo ni muhimu katika miili yetu. Hata hivyo mbegu za flax ni mbegu maarufu kwa kuwa na estrogen ambayo ni sawa kabisa na homoni ya estrogen iliyoko katika miili ya wanawake.  Flax seeds zina kiwango cha phytoestrogens mara tatu zaidi...

Maradhi Yanayotibiwa na Habbat Soda (BLACK SEEDS)

Picha
Yafuatayo hapa chini ni baadhi ya matatizo na magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kirahisi kwa kutumia Habbat-Sawdaa.  Vipele (chunusi) Na Ngozi:    Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.  Upara (Alopeshia):    Sugua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika mabaka yanayokusumuba.  Pumu:    Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.  Kuumwa kwa Mgongo (Sehemu ya Chini):    Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufu...

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

Picha
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito).  Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.  Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni.  Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe ...

USHAURI MUHIMU UKIWA UKO PEKE YAKO NJIANI NA UMEPATWA NA SHAMBULIA LA MOYO (HEART ATTACK) CHUKUWA TAHADHARI. 

Picha
Chukulia ni muda wa saa 1:25 usiku unarudi nyumbani peke yako, baada ya kazi ngumu zusizo za kawaida ofisini.Umechoka sana, una hasira na umechanganikiwa.Ghafla unajisikia maumivu makali kifuani yanaelekea mkononi na hata kwenye Taya. Upo umbali wa kama km5 tu kufika Hospitali iliyo karibu na kwako.Bahati mbaya hujui kama utaweza kufika kwa vunavyojisikia.Ulishafundishwa kumfanyia mtu CPR, lkn aliyekufundisha hakuwaambia unaweza kujifanyia mwenyewe. JINSI YA KIJUSAIDIA UNAPOPATWA NA SHAMBULIO LA MOYO UKIWA PEKE YAKO . Kwa kuwa watu wengi hupatwa na Shambulio la Moyo wakiwa peke yao bila msaada wowote, mtu ambaye mapigo yake ya Moyo hayako sawa na anaanza kuhisi kuzimia, au zimebaki sekunde 10 tu kabla hajapoteza fahamu.Hata hivyo, waathirika hawa wanaweza kujisaidia kwa kujikoholesha mfululizo. Avute pumzi ndefu kila unapo jikoholesha, na kikohozi lazima kiwe cha ndani mfululizo mpaka makohozi yatoke ndani ya kifua.Kikohozi hicho kiendelee mpaka utakapopata msaada au mpaka mapigo y...