FAIDA ZA TUNDA LA STAFELI
Baadhi ya dawa za hospitali huathiri njia ya chakula na kumsababishia mgonjwa ukosefu wa choo kwa muda mrefu, lakini stafeli likitumika hurekebisha hali hiyo na kumsaidia mgonjwa kupata choo kama kawaida. Vilevile, baadhi ya dawa za hospitali za saratani hudhoofisha kinga ya mwili, lakini virutubisho vilivyomo kwenye stafeli, hasa vitamin C, huzifanya kinga kuwa imara na hivyo kuziimarisha hivyo kumuepusha mtu kupatwa na maambukizi mengine, kama ya njia ya mkojo, mafua na kikohozi cha mara kwa mara. FAIDA ZINGINE ZA STAFELI NI KAMA ZIFUATAVYO: Hutoa nafuu ya kipanda uso. Kirutubisho aina ya Riboflavin kilichomo kwenye stafeli, husadia kutoa nafuu kwa ugonjwa wa kichwa cha kipanda usoni. HUZUIA UGONJWA WA ANEMIA Madini ya chuma (iron) yaliyomo kwenye stafeli, hufaa sana katika kuzuia ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia). HUTIBU MAGONJWA YA INI Juisi ya stafeli inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu matatizo ya kwenye ini na uvimbe kwenye kibofu cha mkojo. HUIMARISHA MIFUPA Stafe...