Dawa ya jino ya asili
Maumivu ya jino ni moja ya maumivu mabaya sana kuyapata, maumivu mengine mabaya zaidi ni maumivu ya sikio. Jino linaweza kupatwa na maumivu ambayo yanaweza kupelekea jino kutoboka na hata kuong’olewa kabisa. Maumivu haya yanaweza kuletwa na maambukizi ya bakteria kutokana na vyakula tunavyokula au kutokusafisha kinywa vizuri kila siku, jino kupata jeraha, magonjwa ya fizi, na udhaifu wa mifupa mwilini mwako kwa ujumla. Maumivu mengi ya jino ni ishara kuwa huna chumvi ya kutosha mwilini, huna maji ya kutosha mwilini na hujishughulishi na mazoezi ya viungo kila mara. Dawa zifuatazo zinaweza kutuliza maumivu ya jino na hata kuliziba kabisa iwapo tayari limeanza kutoboka. 1. Asali yenye mdalasini dawa ya jino Asali yenye mdalasini Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na vijiko vikubwa viwili vya asali mbichi na upake kidogo kidogo juu ya jino linalouma mara kadhaa kwa siku mpaka maumivu yatakapopotea. 2. Aloe vera (mshubiri) dawa ya jino Aloe Vera (...